MABASI YA MWENDOKASI YAANZA ROUTE MPYA MUHIMBILI LEO
Kampuni ya mabasi ya mwendo kasi jijini Dar es salaam ( UDART) imeanzisha route mpya ya MUHIMBILI leo , Hii ni kutokana na tukio lililojitokeza siku mbili tatu zilizopita .. Tukio hilo lilijitokeza eneo la Mbezi Luis jijini baada ya Mwanamke mmoja kusubiri sana basi linaloelekea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa ajili ya Matibabu. alifariki baada ya kuchelewa kupata usafiri unaolekea hospitalini hapo
kwa kutambua usumbufu huu wanaopata Abiria wanaenda Hospitalini hapo wameamua kufungua au kuanzisha route hii mpya .... Ambayo itakua inaanzia Gerezani na kuelekea Muhimbili , kwa abiria wanaotokea Mbezi, Kimara ,Ubungo na Kivukoni watalazimika kushuka kituo cha Mabasi ya mwendokasi Fire na kusubiri basi zinazotoka Gerezani . Abiria wanaonga magari hawatalipa tena nauli badala yake watatumia tiketi zao za awali walizokata .... Amesema Meneja mahusiano UDART




Post a Comment