JUVENTUS YATINGA FAINALI ULAYA
Timu ya klabu ya Juventus hatimae imetinga fainali ya Klabu bingwa barani ulaya mwaka 2017 ..... Jana usiku baada ya kumtundika Monaco katika uwanja wa Juventus
Wakiwa wanaongoza 2-0 katika awamu ya kwanza ya mechi ,timu hiyo ya Itali iliongeza jumla ya mabao wakati mshambuliaji wao Mario Mandzukic alipofunga .
Dani Alvez aliongeza bao la pili baada ya kipa Danijel Sabusics kuupangua mpira ulioanguka mbele yake.
Kylie Mbappe alifunga krosi iliopigwa katika kimo cha nyoka ya Joao Moutinho ili kufunga bao la kufutia machozi, lakini klabu hiyo ya ligi ya daraja la kwanza haikuweza kufunga zaidi ya bao moja.
Juventus ambao hawajashinda kombe hilo tangu 1996 na waliopoteza katika fainali ya mwaka 2015 dhidi ya Barcelona watakabiliana na Real Madrid au Atletico Madrid katika uwanja wa Cardiff mnamo tarehe 3 mwezi Juni.
Klabu hiyo sasa yamsubiri mshindi wa leo .. katika mechi kati ya Real Madrid na Atletico Madrid , klabu ya real madrid leo itakua ugenini wakivaana na mahasimu wao




Post a Comment